MR MONEY MZEE WA UNAFUU WA UHAKIKA

MR MONEY MZEE WA UNAFUU WA UHAKIKA
............................................................................................

FAIDIKA NA ZOTE KALI KATIKA MSIMU WA SIKUKUU.

FAIDIKA NA ZOTE KALI KATIKA MSIMU WA SIKUKUU.
......................................................................................................................

DSTV BOMBA

DSTV BOMBA
..............................................

TUUNGANE KWA PAMOJA

TUUNGANE KWA PAMOJA
.............................................................

KIJUKUU BLOG TEAM SISI TUTAWALINDA WEWE JE?

KIJUKUU BLOG TEAM SISI TUTAWALINDA WEWE JE?
...................................................................

KARIBU KAHAMA KWA MALAZI SAFI.

KARIBU KAHAMA KWA MALAZI SAFI.
PLACE TOBE

NJOO UPENDEZE NASI

NJOO UPENDEZE NASI
TUPIGIE 0758-762255

WAUZAJI WA VIFAA VYA SHULE MJINI BUKOBA.

WAUZAJI WA VIFAA VYA SHULE MJINI BUKOBA.
....................................................................

'

'
'

Kwa Habari Makini za Kila siku, Michezo,Burudani,Biashara,Matukio na Habari za Kimataifa tembelea hapa, pia kwa matangazo wasiliana nasi  Piga 0767942570 au 0786942470

Tuesday, December 6, 2016

Waziri Simbachawene atoa maagizo kuhusu wamachinga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa, wilaya na mamlaka ya Serikali za mitaa kuwatafutia wamachinga maeneo rafiki ya kufanyia baishara badala ya kuwabughudhi kwa kuwaondoa katika maeneo wanayofanyia biashara.

Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni agizo kutoka kwa Rais John Magufuli ambaye amesema haridhishwi na namna mamlaka husika zinavyoshughulikia suala la wamachinga ambapo amewataka kuangalia utaratibu mzuri utakaotumika kuwaondoa katika maeneo yao, na ikibidi kuwatafutia maeneo bora zaidi ya hayo.

Aidha amewataka watendaji hao kuangalia utaratibu mzuri wa kuwashirikisha wajasiriamali ili kupata ufumbuzi ulio shirikishi zaidi kwa kuanzia ni vema yakatengwa maeneo ya katikati ya miji yenye wateja wa bidhaa zinazouzwa kwa kuangalia uwezekano wa kufunga mtaa japo mmoja ili kutumikakwa kazi za kimachinga.

Kwa mujibu wa Waziri Simbachawene serikali imesikia kilio cha wafanyabiashara wadogo wanaotozwa ushuru mbalimbali kulingana na biashara zao tozo ambazo zinawadidimiza zaidi.

Bwawa la Mindu Morogoro lagundulika kuwa na kipindupindu

Siku moja baada ya mkuu wa wilaya Morogoro Regina Chonjo kuzuia matumizi ya bwawa la mindu  kwa madai kwamba chanzo hicho cha maji kina vimelea vya kipindupindu, diwani wa kata ya Mindu, Hamis Msasa amepingana na maamuzi hayo  na kuruhusu wananchi kutumia maji ya bwawa hilo kwa matumizi yao ya  kawaida  .

Akiongea na channel ten  diwan  wa kata ya mindu Hamisi Msasa amesema kuwa  kusimamishwa kwa shughuli za kibinadamu  ikiwemo uvuzi  imekuwa kero kubwa kwa wananchi wake  hasa wakina mama wanaotegemea chanzo hicho  kwa matumizi ya maji huku wananchi hao wakida kuwa  shughuli zote zinazofanyika  katika bwawa hilo zipo kiharali na  wamekuwa wakilinda chanzo hicho  zidi ya waharamia na kumutaka mkuu wa wilaya kufanya  mazungumuzo  na wananchi kabla ya uamuzi  ambao unaweza kuwaasili .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya morogoro mjini Regina Chonjo amesema kuwa kutokana na hari iliyopo ya dalili za ugonjwa wa kipindu pindu hataweza kuruhusu bwawa hilo litumike mpaka pale watakapo jilizisha kuwa hali imetengamaa kwani katika utafiti uliofanyika asilimia kubwa ya maji ya bwawa la mindu yana chembechembe ya  kuambukiza magonjwa ya tumbo.

Hospitali ya kisasa Chanika kuzinduliwa Mwezi ujao

Hospitali kubwa ya kisasa inayojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Korea – Koica inatarajiwa kufunguliwa mwezi Februari mwakani baada ya ujenzi wake kukamilika ambapo hivi sasa imefikia asilimia 80.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanya ziara katika Hospitali hiyo iliyopo Chanika jijini humo ambayo ni mahsusi kwa ajili ya  kutoa huduma za mama na mtoto, upasuaji, huduma za dharura ikiwa ni pamoja na kuhudumia wagonjwa mbali mbali zaidi ya elfu moja kwa Siku.

Amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo kutasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali za Amana na Temeke kwa kuwa kutakuwa na madaktari Bingwa kutoka hapa nchini pamoja na wale watakaotoka Korea ambapo pia wataendesha mafunzo maalum hapa nchini.

Makonda amesema pamoja na ujenzi wa hospitali hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dk.Magufuli lakini hospitali nyingine zinatarajiwa kujengwa kwenye wilaya mpya za Kigamboni na Ubungo, lengo likiwa kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma za afya katika jiji la Dar es salaam na kuondoa  Msongamano kwenye Hospitali za Rufaa.

Ligi Kuu Vodacom Kuanza Kutimua Vumbi Desemba 17, Simba Na Yanga Februari 18 Mwakani

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Alfred Lucas

LIGI kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kwa duru la pili kuanzia Desemnba 17, huku timu zikishauriwa kukamilisha usajili kwa wakati huku Yanga na Simba kuumana Februari 18 2017..

Dirisha la usajili lililofunguliwa Novemba 15 linatarajiwa kufungwa Desemba 15 na timu zote zimeopewa mwongozo wa kutumia mfumo wa ule ule wa kutumia mtandao katika kuwasilisha majina hayo usiku wa Desemba 15.

Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa ligi inatarajiwa kuanza Desemba 17 kwa mechi nne kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini.

Lucas amesema kuwa kwa sasa ratiba hii imezingatia kalenda ya michezo ya kimataifa, kombe la mapinduzi na kombe la Shirikisho ilihali hawajaweza kuweka ratiba ya michezo ya kimataifa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kwani ratiba ya Shirikisho la Mpira Afrika bado hawajaweka raiba wazi.

Katika ratiba hiyo, Kikosi cha Simba kitaanzia ugenini kuvaana Ndanda huku mabingwa watetezi Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa kuumana na JKT Ruvu na Azam watakuwa ugeninio dhidi ya African Lyon.

Waziri Mkuu ajiuzulu, ili kujikita na Kampeni Urafansa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amejiuzulu wadhifa wake, ili kujikita katika kampeni za kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka ujao. Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve, ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya.

Valls amejiuzulu siku moja baada ya kutangaza nia yake ya kugombea urais, baada ya Rais Francois Hollande kuamua kutogombea muhula wa pili kwa tiketi ya chama chao cha kisoshalisti.

Kiama chaikumba TASAF, maafisa 111 watumbuliwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kuwasimamisha kazi mara moja maafisa ushauri na mipango 106 katika ngazi ya halmashauri nchini.

Wengine wanaopaswa kusimamishwa ni pamoja na maafisa 5 wa ngazi za juu wa makao makuu ya TASAF.

Maafisa hao wanaondolewa kazini mara baada ya kuingiza kaya zisizo na sifa ya kupokea ruzuku serikalini na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 6.4.

Jambo hilo limemlazima Mhe. Kairuki kuamuru wachunguzwe ndani ya mwezi mmoja huku Meneja na Mkurugenzi wa Uratibu pamoja na maafisa watano waandamizi wa makao makuu ya TASAF nao wakisimamishwa kazi.

Mhe. Kairuki amesema asilimia 28.2 ya watanzania wote ni masikini sana na kwamba serikali imekwisha kutumia zaidi ya shilingi bilioni 391 kwa ajili ya kuhudumia awamu ya tatu ya mpango wa kunusuru kaya masikini na kwa sasa inajikita kuhakikisha kuwa wanaonufaika na ruzuku hiyo ni walengwa pekee.

Alichokiandika Darassa baada ya dereva kukamatwa akicheza wimbo wake huku akiendesha gari

Msanii wa Bongofleva Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na hit single ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ile video iliyosambaa ikionesha vijana wakicheza wimbo wake  huku dereva akiacha  gari likienda.

Vijana hao wamekamatwa na polisi na Darassa ameamua kutoa mawazo yake kuhusiana na kitendo hicho ambacho kimewafanya vijana hao kukamatwa na polisi Itigi Singida, Darassa ametuamia account yake ya instagram kuandika ujumbe kuoneshwa kuguswa na

“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie 🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“

Majaliwa awakabidhi wananchi shamba la mifugo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemkabidhi hati ya shamba la mifugo la Manyara, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya baada ya kubadilisha umiliki wa shamba hilo.

Umiliki ulibadilishwa kutoka Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) ambayo mwenyekiti wa bodi yake ni Mbunge wa zamani wa Monduli, Edward Lowassa kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili vya Elesilalei na Ortukai vya kata ya Elesilalei, eneo la Makuyuni, wilayani hapa.

Hatua ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi ni baada ya kilio cha muda mrefu kwa wananchi hao kudai kuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliagiza shamba hilo ligawiwe kwa wananchi lakini haikuwa hivyo, badala yake watu wachache walijimilikisha kinyemela chini ya wenyekiti wa bodi ya TLCT.

Majaliwa alitangaza kukabidhiwa hati hiyo wakati alipomtembelea mwanzilishi wa Shule ya Msingi Laibon, Leshuko ole Mapii, kata ya Elesilalei.

Alifika kujionea hali halisi ya mwamko wa elimu kwa mzee huyo ambaye wajukuu zake na watoto wake zaidi ya 102 wanasoma shuleni hapo pamoja na watoto wengine wanaotoka jirani na eneo hilo.

Alisema serikali imeamua kurudisha shamba hilo kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili baada ya Baraza la Madiwani na uongozi wa wilaya hiyo ya Monduli kuridhia kwa pamoja umiliki wa shamba hilo kurudi kwa wananchi.

Alisema shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 44,930 lilikuwa likimilikiwa na TLCT linalofadhiliwa na Shirika la African Wildlife (AWF), hivi sasa ni mali ya wananchi na halmashauri ya Monduli ndio wataamua kupanga matumizi bora ya ardhi.

Alisema nyaraka zinazoonesha kuwa shamba hilo lililotolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu mwaka 1999 kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini hakuna kilimo chochote hapo na badala yake TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.

"Sasa namkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli hati hii na kuanzia leo(jana) umiliki wa shamba hilo utakuwa chini ya halmashauri na wananchi mtaamua kupanga matumizi bora ya ardhi katika shamba hili mliloteseka nalo kwa muda mrefu," alisema.

Alisema serikali itawanyang'anya mashamba wale wote wanaomiliki bila ya kuyaendeleza kwa kuwapa wananchi na kuhoji ni kwa nini wenye fedha kuchukua mashamba mkubwa bila ya kuyaendeleza.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kabla ya ujio wa Waziri Mkuu, alifanya ziara katika shamba hilo na kuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli, mkoani Arusha na baraza la madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha wanabadilisha umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji husika kama Rais mstaafu, Benjamini Mkapa, alivyoagiza.

Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isack Joseph kwa nyakati tofauti waliishukuru serikali kwa uamuzi huo na kuipongeza serikali kwa kujali maslahi ya wananchi wake.

Mkurugenzi wa TLCT, Boniface Ngimojiro alipopewa nafasi ya kusema neno kwa wananchi hao, alisema taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya wadhamini yenye wajumbe wanane wakiongozwa na Mbunge wa zamani wa Monduli, Edward Lowassa kama mwenyekiti wa bodi hiyo.

Aidha alikiri kupata amri ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili na kusisitiza kuwa kwa sasa ameridhia shamba hilo kumilikiwa na wananchi.

Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe, alisema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ndani ya shamba hilo pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye shamba hilo ikiwemo shule, zahanati, ufugaji wa kisasa na machinjio.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, aliwasihi wananchi hao kuheshimu njia za mapito ya wanyama katika eneo hilo ambalo wanyamapori kutoka hifadhi za Tarangire, Manyara na Ngorongoro wanalitumia kwa ajili ya kupita kwenye hifadhi hizo mara kwa mara.